Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 1:46 pm

NEWS: ZIFAHAMU TIMU 6 ZA ULAYA ZINAZOMTAKA SAMATTA KWA SASA

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania na Mshambuliaji nyota wa mabingwa wa ligi ya Ubelgiji klabu ya KRC Genk Mbwana Samatta huenda akajiunga na moja kati ya ligi kuu mbili kubwa barani ulaya ambazo ni Ligi Kuu ya England (Primia) au ligi kuu ya Hispania La liga kwa msimu ujao(2019/2020).

Samatta, alisema kuwa kuna vilabu sita vya Ligi ya Primia ambavyo vinawania kutaka saini yake.

Samatta na tuzo

"Kwa sasa sipo katika nafasi nzuri ya kuelezea ni klabu gani lakini pia kuna klabu nyingine mbili kutoka Hispania ambazo zimekuwa zikiisaka saini yangu. Hata hivyo, mimi ndoto zangu ni kucheza katika Ligi Kuu ya England," Samatta ameliambia gazeti la Mwananchi.

Lakini taarifa za MuakilishiTZ tulizozipata kutaka kwa mmoja wa watu wa karibu wa Mtanzania huyo alisema kuwa vilabu vikubwa vinavyotaka saini ya Samatta ni vingi kama Everton, WestHam, Cardiff na Burnley zote hizi kutoka Uingereza " nikwambia kitu yaani vila ni vingi sana kwasasa vinataka huduma ya Samatta kwa mfano Everton, WestHam, Cardiff na Burnley ingawa hawa Cardiff wameshuka daraja lakini bado wanamuwinda hivyohivyo" amesema Ndugu huyo wa Samatta

"kuna timu mbili za La liga wale Villarreal na Celta Vigo nao wako moto sana kumtaka Samatta" aliongezea Ndugu huyo

Jina la Samatta limekuwa likiimbwa na mashabiki wa Genk, na wamekuwa wakimuomba mshambuliaji huyo kusalia klabuni hapo kucheza ligi ya Mabingwa Ulaya. Samatta ameiambia Mwananchi kuwa moyo wake upo England japo kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa ni kitu cha kutamanisha pia.

Samatta alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe Januari 2016 ambapo alitia saini mkataba wa kumuweka katika klabu hiyo hadi msimu wa 2019/20.

Amesalia na miezi 12 kabla ya mkataba wake kumalizika.

Samatta alihamia Ubelgiji mwaka mmoja baada ya kutawazwa mchezaji bora wa mwaka Mwafrika aliyekuwa anacheza ligi za barani Afrika mwaka 2015.

Alishinda vikombe sita vikuu akiwa na TP Mazembe ikiwa ni pamoja na kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 2015 kabla ya kuondoka.