- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZAIDI YA WATU LAKI MBILI KUPOTEZA MAISHA KWA MAGONJWA MBALIMBALI.
DODOMA: ZAIDI ya watu laki mbili nchini wamepoteza maisha ndani ya muda wa miaka kumi kutokana na magonjwa mbalimbali kufuatia taarifa kutoka Taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini (NIMR).
Akizungumza katika warsha yenye lengo la kuwasilisha taarifa ambazo taasisi hiyo imekusanya pamoja na kujadili jinsi ya kuboresha huduma ya afya nchini katika hospitali ya rufaa ya mkoani Dodoma Dokta Leonard Mboera kutoka Taasisi hiyo alisema kuwa utafiti huo ulifanyika katika hospitali 39 nchini kuanzia mwaka 2006 hadi 2016.
‘’Tulifanya Katika hospitaliza rufaa 39 za Tanzania bara na ilikujuisha Hospitali ya taifaMuhimbili, hospital za rufaa za kanda , Mbeya, Bugando, na kcm na ilihusisha vilevile zilihusisha hospitali za mikoa 20 na asilimia 10 hospital za wilaya 11’’ alisema.
‘’Kikubwa kilichohusisha kwenye Twakimu nanaomba nisisitize tuliangalia takwimu za miaka 10 na siyo tulikkaa kwenye hospital hizo kwa miaka 10 kwahiyo takwimu hizi zinapatikana katika taarifa za hospitali baada ya kufanyia uchanganuzi tulipata vifo vyazaidi ya laki mbili’’ alisema
Dk Leonard alisema changamoto kubwa katika hospitali nchini ni upatikanaji wa Twakwimu ambapo hospitali nyingi zinatumia mfumo wa analogi katika kutunza takwimu hizo hali inayosababisha upotevu wa takwimu hizo.
Aidha aliwataka madaktari mbalimbali nchini kuweza kuhifadhi takwimu hizo katika mfumo wa kidigitali na sio kwa njia ya analogi ili kuepuka upotevu wa takwimu hizo.