Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:28 pm

NEWS: ZAIDI YA WATU 40 WAMEUWAWA KATIKA SHAMBULIO LA MISIKITI 2 NEWZEALAND

Zaidi ya Watu 40 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa vibaya mno baada ya watu wanne kufanya mashambulizi katika msikiti miwili katika mji wa Christchurch, Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amesema.

Image result for New Zealand two shootings at two mosques in Christchurch

Maofisa wa polisi wametumwa katikati mwa jiji la Christchurch baada ya mashambulizi ya risasi katika misikiti miwili nchini New Zealand. Polisi, ambayo inasema "watu wengi wameuawa, imewakamata watu kadhaa.

Image result for New Zealand two shootings at two mosques in Christchurch

Kwa mujibu wa chanzo cha polisi katika eneo la tukio, vizuizi vimeanza kuondolewa kwenye barabara za mji huo mara baada ya polisi kutangaza kuwa wamekamata watu wanne na mabomu yaliyotengenezwa kienyeji.

Related image

"Watu wanne, wanaume watatu na mwanamke mmoja, wanashikiliwa na polisi, " amesema, mkuu wa polisi katika eneo hilo Mike Bush, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, huku akibiani kwamba jeshi lilitegua kilipuzi kilichopatikana katika magari ya watuhumiwa.

Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison amesema mojawapo ya waliokamatwa ni raia wa Australia.

Amemtaja mshukiwa wa shambulio hilo kuwa "gaidi mwenye itikadi kali za mrengo wa kulia".

Awali mkuu wa pilisi katika mji wa Christchurch amesema watu waliouawa ni wengi, lakini hakutaja idadi.