- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZAIDI YA WATU 36 WAMEUWAWA KWENYE SHAMBULIO LA HOTEL UFILIPINO
MANILA: Mili ya watu 36 imegunduliwa leo Ijumaa Juni 2katika hoteli Resorts World Manila casino nchini Ufilipino ilioshambuliwa na mtu aliyejihami kwa silaha kabla ya kujiua. Polisi katika mji wa Manila inasema kwamba mtu ambaye alitekeleza shambulizi hilo pengine ni raia wa kigeni.
Watu thelathini na sita wameuawa," alisema kwenye kituo cha CNN nchini Ufilipino mkuu wa polisi ya mji wa Manila, Oscar Albayalde baada ya shambulio hilo lililotokea usiku kuamkia leo Ijumaa katika hoteli Resorts World Manila, hoteli inayopatikana karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila. Awali afisa mwengine wa polisi, Tomas Apolinaro alisema watu 34 waliuawa katika shambulio hilo.
Polisi wanasema kuwa, mtu aliyekuwa amejihami kwa silaha alivamia ukumbi wa Casino katika jiji hilo na kuanza kuwapiga watu risasi.
Aidha, wanasema mtu ambaye alitekeleza shambulizi hilo alijiuawa kwa kujipiga risasi baada ya kuanza kukabiliana na maafisa wa usalama.
Ripoti zinasema kuwa, watu wengi walipoteza maisha baada ya kuathiriwa na moshi katika ukumbi huo baada ya kushika moto kutokana na makabiliano hayo.
Watu zaidi ya 50 wamejeruhiwa katika shambulizi hili ambalo linachunguzwa kama la kigaidi au kama ni uhalifu wa kawaida uliofanyika.