Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:40 am

NEWS: ZAIDI YA WATU 10000 KUPOTEZA MAISHA KILA MWAKA KWA TATIZO LA USUGU WA DAWA

DODOMA: Zaidi ya watu millioni kumi kila mwaka duniani kote kupoteza maisha kwa tatizo la usugu wa dawa linalotokana na matumizi mabaya ya dawa yasiyozingatia ushauri wa kitabibu.

Hayo yamesemwa na Rais wa chama cha wanafunzi wafamasia Tanzania (TAPSA)Erick Venant wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kujitolea ijulikana kama '' Tapsa tokomeza usugu wa dawa amr holiday campaign'' uliofanyika katika shule ya sekondari ya wasichana msalato mjini hapa.

Venant amesema kuwa chama hicho kinalenga kutoa elimu kwa jamii kuelewa maana ya usugu wa dawa na jinsi tabia na kwamba tatizo hili linatokana na tabia mbalimbali kamakutokukamilisha dozi,matumizi ya dawa bila kupima na kupata ushauri wa kitaalamu.

“Jamii inapaswa kutambua kuwa kununua dawa bila cheti cha daktarina pia matumizi ya dawa za binadamu kwa mifugo hizi ni tabia katika jamii yetu nazimechangia sana kuwepo kwa tatizo hili”anasema.

Aidha Rais amesema Kampeni ya kupambana na tatizo la usugu wa dawa nchini ni nguzo muhimu ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na usugu wa dawa za binadamu haswa antibayotikia ambazo zinakadiriwa kuongezeka hadi kufikia watu million kumi kila mwaka .

Hata hivyo amesema ,Tangu kuzinduliwa kwa kampenihii ya kujitoleaTAPSA imeweza kuzifikia shule za sekondari89 katika mikoa 18 ya Tanzania ambapo imeweza kutoa elimu kupitia vyombo vya habari katika mikoa mbalimbali kote Tanzania bara na Zanzibar.

“Tunatumia vyombo vya habari kuhakikisha tunafikisha ujumbe kote nchini ,hata hivyo Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la afya duniani(WHO) mwezi uliopita(Septemba) inaoneshausugu wa dawa za kifua kikukuu peke yake husababisha vifo 250000 kila mwaka na hivyo tunapaswa kupambana zaidi”amesema.

Chama cha wanafunzi wa famasi Tanzania (TAPSA) kilianzishwa mwezi Agosti mwaka 1987 katika chuo kikuu cha Dar Es Salaam kikijulikana kama ADUPS (Association of Dar Es Salaam University PharmaceuticalStudents) ambapo kwasasa kina matawi nane katika vyuo vya CUHAS(Catholic University of Health and Allied Sciences) Muhimbili University of Health and Allied Sciences(MUHAS), Ruaha Catholic University(RUCU),State University of Zanzibar(SUZA),St.Johns University of Tanzania(SJUT),St.FrancisUniversity of Health and Allied Sciences(SFUCHAS) na University of Dodoma(UDOM).