Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 6:29 pm

NEWS: ZAIDI YA VIJANA MILION 53 HAWANA AJIRA NCHINI.

DODOMA: Waziri wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Majaliwa kassim Majaliwa amezindua miongozo ya mafunzo kazini ambapo lengo la miongozo hiyo ni Kutatua tatizo la ukosefu wa ajira nchini.

Uzinduzi huo umefanyika leo mjini Dodoma , Majaliwa Amesema ripoti ya mwaka 2017 ya shirika la kazi duniani [ILO] inaonesha kuwa zaidi ya watu million 201 sawa na asilimia 5.8 ya watu wanaostahili kufanya kazi hawana kazi, Kati ya watu hao vijana ni million 53.6 sawa na asilimia 13.7.

Ameongeza kuwa kwa upande wa Tanzania utafiti wa nguvu kazi wa mwaka 2014 unaonesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira nchini ni sawa na sailimia 10.3 na kwa vijana nia asilimia 11.7.

Waziri Majaliwa amesema serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 iliandaa na kuanza kutekeleza program ya miaka mitano ya taifa ya kukuzaujuziambayo itatoa mafunzoya kukuza ujuzi kwa takriban vijana million 4 ili kuziba pengo la ujuzi lili[o nchini kwa mujibu wa utafiti wa nguvu kazi ya mwaka 2014.

Naye Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Joakim Mhagama amesema miongozo hiyo kwa uanangezi nikusimamia utaratibu Kwa wahitimu wanapokuwa kwenye mafunzo yao, kuwa na muda maalumu kwa uanangezi wahitimu, nikuweka bayana kati ya mwajiri na mfanyakazi.

Kwa upande wake katibu mkuu Wa TUCTAYahaya Msingwa ameiomba serikalikuwa vyuo vya ufundi stadi [VETA] Kuhamishiwa katika wizara ya elimu , elimu za kati zizingatie zaidi kurekebisha mtaala wa elimu ili iweze kufikia fursa ya kujiajiri na si kuajiriwa.

Programu hiyo ilianza kutengenezwa mwaka 2015/2016 ambapo kauli mbiu ya ‘’ miongozo hiyo ni nguvukazi ya kitaifa kiujuzi na kuajirika’’