Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:28 am

NEWS: ZAIDI YA MILIONI 28 ULIPWA KILA MWEZI LUSHOTO

Dodoma: HALMASHAURI ya wilaya ya Lushoto inatumia zaidi ya shilingi milioni 28 kulipa mishahara ya watumishi kila mwezi.Bunge limeelezwa

Mbunge wa Mlalo Rashid Shangazi alitoa kauli hiyo wakati akiuliza swali Bungeni ambapo alisema,huo ni mzigo kwa Halmashauri ambapo kazi hiyo ilipaswa kufanywa na Hazina kupitia Utumishi.


"Je,ni lini Serikali itawatua wananchi wa Lushoto mzigo huo.?" amehoji Shangazi

Akijibu swali hilo,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angela Kairuki alisema,katika Halmashauri ya wilaya wapo watumishi wanaolipwa kutoka Serikali Kuu na watumishi wanaolipwa kutoka katika vyanzo vya Mapato ya ndani ya Halmashauri husika 'own source'.



Amesema ,utaratibu huo ulianzoshwa baada ya kuonekana kuwepo kwa mahitaji maalum yanayowasilishwa na waajiri kutaka watumishi wa ziada tofauti na ukomo wa bajeti ya mishahara ya Serikali huku akisema,Halamshauri ya wilaya ya Lushoto inao mzigo huo kwa kuwa iliona inao uwezo wa kuwalipa watumishi wake kupitia Mapato yake ya ndani.

"Kwa upande wa Halamshauri ya wilaya ya Lushoto kuna jumla ya watumishi 116 ambao waliajiriwa katika utaratibu huo 'own source ' kwa kuwa Halmashauri hiyo ilitoa inaweza kumudu gharama za kuwalipa mishahara kutokana na vyanzo vyake vya mapato ya ndani." amesema Kairuki