- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZAIDI YA MADEREVA 1500 KUAJIRIWA NA BOMBA LA MAFUTA.
Hayo yameelezwa na Harshil Davda, Ofisa Usafirishaji wa Kampuni ya Simba Logistics inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu wa Tanzania, Azim Dewji. Davda aliyasema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam, wakati wa kusainiwa kwa makubaliano ya kufanya kazi pamoja baina ya Chama cha Watoa Huduma katika Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) na wenzao wa Uganda (AUGOS).
Alisema wapo tayari kuanza kazi na pia wananunua magari zaidi kwa kuwa mradi unahitaji magari yenye uwezo wa kufanya kazi kwa uhakika na kwamba yanahitajika kati ya magari 1,000 na 1,500.
Kwa sasa, Simba Logistics ina malori zaidi ya 300 yanayofanya kazi katika nchi za Afrika Mashariki na Kati, yakisafirisha mafuta na bidhaa nyingine. Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa AUGOS, Emmanuel Mugarura alisisitiza mshikamano na ushirikiano wa kweli baina ya nchi hizo, ili wafanye kazi kwa ubora hivyo kujitengenezea mazingira mazuri ya kuaminiwa na kupewa kazi zaidi, badala ya kusubiri kila kitu kifanywe na kampuni na raia kutoka China, Ulaya au Marekani.
“Tuitumie faida hii kuunganisha nguvu. Lazima tuione faida ya kuwa na ushirikiano wa Afrika Mashariki,” alisema Mugarura. Mradi wa bomba hilo unaotarajiwa kukamilika mwaka 2020, unatarajiwa kuwa na urefu wa kilometa 1,445 kati ya hizo zikitambaa katika ardhi ya Tanzania ambako itapita katika mikoa minane yenye wilaya 24 na vijiji 184.
Tanzania litapita katika mikoa ya Kagera, Geita, Simiyu,Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga. Nchini Uganda, litaanzia Ziwa Albert (Hoima) kwa umbali wa kilometa 296 mpaka mpakani mwa Tanzania.
Wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo kijijini Chongoleani, ilielezwa kuwa, bomba hilo litavutia mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda pamoja na ajira 11,000 za moja kwa moja na vibarua takribani 30,000.