Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 5:34 pm

NEWS: ZAIDI YA HATI MILIKI ZA KIMILA 400,761 ZATOLEWA KWA WANANCHI

DODOMA: ZAIDI ya hati miliki za kimila 400,761 zimeshatolewa kwa wananchi mpaka sasa.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ANGELINA MABULA amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum BUPE MWAKANG`ATA.

Katika swali lake mbunge huyo ametaka kujua serikali inawasaidiaje wananchi hasa wanawake kwa kuzungumza na Benki ili zikubali kupokea hati za hakimiliki za kimila kama dhamana ya mkopo.


Waziri Mabula amesema kwa mujibu wa kifungu cha 18(1) cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999 hati za hakimiliki za kimila zina hadhi sawa na hati inayotolewa na kamishna wa ardhi.


Amesema hadi sasa Hati za Hakimiliki za kimila zimewezesha wananchi kupata mikopo yenye thamani ya takribani bilioni 59 kutoka taasisi mbalimbali za fedha.

Hata hivyo amesema Wizara kwa kupitia marekebisho ya Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 yanayoendelea inaangalia uwezekano wa kuondoa vikwazo vinavyozuia uuzaji wa dhamana pale mkopaji anaposhindwa kurejesha mkopo pamoja na kuzungumza na taasisi za fedha.