- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: YALIYOJIRI KESI YA TUNDU LISSU DHIDI YA SPIKA NDUGAI
Leo Agosti 15, 2019 imenguruma kesi ya aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, dhidi ya maamuzi ya Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai ya kumvua ubunge wake ambapo Lissu ameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam kutoa amri ya kusitisha zoezi la kuapishwa kwa mbunge mteule wa jimbo hilo, Miraji Mtaturu, ambaye alichaguliwa takriban mwezi mmoja uliopita.
Jopo la wanasheria wanne wanaomtetea Lissu limewasilisha maombi matano ya mlalamikaji , wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala katika shauri la madai nambari 18 la mwaka 2019, dhidi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na mwanasheria mkuu wa serikali, ili apate amri ya mahakama kuhusiana na kuvuliwa ubunge wake aliotumikia kwa takriban mwaka mmoja na nusu kabla ya kupigwa risasi katika mji mkuu wa Tanzania, Dodoma.
Photo @dw
Lissu anaitaka Mahakama Kuu kutoa amri kadhaa ikiwemo ya kumuamuru Spika wa Bunge Job Ndugai kuwasilisha mahakamani taarifa ya uamuzi wa kumvua ubunge aliyoitoa bungeni, ili iweze kuupitia na kisha iamuru kuutengua na kuutupilia mbali.
Miongoni mwa maombi mengine ni mahakama imwamuru Spika ampatie Lissu nakala ya taarifa ya kumvua ubunge pamoja na amri ya kusitishwa kuapishwa kwa mbunge mteule wa jimbo hilo, Miraji Mtaturu, wa Chama cha Mapinduzi CCM, ambaye alitangazwa kuwa mbunge bila kupingwa mwezi uliopita.
Lakini ombi hilo limepingwa vikali na jopo la mawakili wa Serikali wakiongozwa na Wakili Vicent Tango, wakidai kuwa kwa sasa sio muda muafaka wa kuanza kulisikiliza. Aidha wameiomba mahakama muda wa siku nane ili waweze kuwasilisha hati ya kiapo kinzani, pamoja na hati ya maelezo kinzani kabla ya maombi hayo kupangiwa siku ya kuanza kusikilizwa rasmi, kwa kuwa shauri hilo linahusisha mhimili mwingine, ambayo ni Bunge, hivyo wanahitaji muda wa kushauriana na Spika ili kuweza kuandaa kiapo kinzani.
Hakimu anayesikiliza shauri hilo, Sirilius Matupa, alihairisha shauri hilo kwa takriban dakika arobaini na tano na kisha kurejea na maamuzi ya kuhairisha shauri hilo hadi tarehe 23 Agosti ambapo atasikiliza maombi ya Lissu, likiwemo la kusitisha zoezi la kuapishwa kwa mbunge mteule na kisha kutoa maamuzi.