- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WIZKID AAMWAGIA SIFA LUKUKI DIAMOND PLATNUMZ
Dar es Salaam. Nyota wa Muziki kutoka nchini Nigeria, Wizkid amempongeza msanii mwenzake kutoka nchini Tanzania Naseib Abdul Maarufu kama DiamandPlatnumz kwa kitendo cha kuandaa tamasha kubwa (WasafiFestival2019) lenyekuwaunganisha wasanii wa Afrika kuwa kitu kimoja, huku akichagiza kuwa ni kitendo cha mfano wa kuigwa kwa wasanii wengine wa Afrika.
Wizkid ameyasema hayo leo Jumatatu Novemba 11, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam ukiwahusisha wasanii walioshiriki tamasha hilo.
Amesema tamasha hilo ni mfano mwingine wa kuonyesha wasanii wa Afrika ni kitu kimoja na wanashirikiana katika kazi.
“Sijaja kwa sababu nampenda Diamond au naipenda Tanzania bali nimekuja kwa sababu ni tamasha ambalo limewaunganisha wasanii wa Afrika.”
“Hii ni hatua kubwa kwa wasanii kushirikiana na kuungana mkono na inavutia kuona wasanii wanashirikiana. Endeleeni kuunga mkono muziki wa Afrika ili ufike mbali zaidi,” amesema .
Kwa upande wa, Tiwa Savage ameisifia Tanzania kuwa ni nchi yenye watu wakarimu na upendo mkubwa kwa wasanii wao.
Amesema ni wakati wa wasanii wa Afrika kushirikiana na kuungana mkono na dunia ijue kuwa Waafrika wako pamoja.
“Nikupongeze Diamond na timu yako kwa kufanya shoo ambayo inaenda kusaidia matibabu ya watoto, ambayo imetuma nafasi ya sisi pia kushiriki,” amesema Katika mkutano huo Diamond kupitia Wasafi Media amewakabidhi tuzo za shukrani wasanii hao akieleza kuwashukuru kwa namna ambavyo wamejitoa kushiriki kwenye tamasha hilo.
Tamasha hilo lilifanyika Jumamosi iliyopita ya Novemba 9, 2019 jijini Dar es Salaam ambapo asilimia 20 ya mapato yatakwenda kugharamikia matibabu ya moyo kwa watoto waliopo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).