- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WIZARA YA AFYA KUJIPANGA KUPUNGUZA ATHARI ZA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA.
DODOMA: Mkurugenzi wa huduma za afya, lishe na ustawi wa jamii kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni tatizo kubwa katika jamii zetu .
Dk Kapologwe ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa 20 wa kitaalam wa kutathimini utekelezaji wa mkakati wa nne wa sekta ya afya uliofanyika leo Jijini Dodoma.
Amesema kuwa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na TAMISEMI pamoja wadau watajadili ili kuweza kupunguza athari za magonjwa hayo kwa jamii ili kuweza kuipunguzia Serikali mzigo wa gharama za matibabu.
Hata hivyo ameendelea kusema madhumuni ya kikao hicho ni kuweka mikakati ya kuhakikisha vituo vya afya vinavyojengwa vinatoa huduma inayostahili na kupunguza vifo vitokana vyo na uzazi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amesema utakua tofauti na mikutano minginekwasababu unapitia mafanikio na changamoto za mipango mikakati iliyowekwa kwamiaka mitano toka mwaka 2015/16 mpaka ifikapo 2020/21 ikiwa ni pamoja na kuweka maazimio ya pamoja ya kukabiliana na changamoto zitakazobainika ili kufikia malengo yaliyowekwa pia kuandaa mkakati wa tano utakaoanza mwaka 2020/21 mpaka 2025/26.
Mkutano huo unaofanyika kila mwaka ulianza mwaka 1999 na kuendelea mpaka leo ambapo wizara ya Afya kazi yake ni kutunga sera na kuzipeleka Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na kwa wadau wa maendeleo kwa ajili ili utekelezaji katika mikoa na Halmashauri zote nchini.
Kauli mbiu ya Mkutano huo ni ‘’Ushirikiano wa wadau ni nguzo muhimu katika utoaji huduma bora za afya ili kufikia malengo kuwa na jamii yenye afya bora na Taifa lenye Maendeleo,’’.