Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 5:30 am

NEWS: W.H.O YAIKOSOA VIKALI TANZANI MAPAMBANO DHIDI YA CORONA

Mkuu wa Shiriki la Afya Duniani (WHO) upande wa bara la Afrika Bi Matshidiso Moeti ameikosoa vikali Serekali ya Tanzania namna ambavyo imelishughulia Gonjwa la Corona.

Bi Moeti anasema kuwa kumekuwa na hofu juu ya kukua kwa kasi ya maambukizi katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

"Kwa hakika tumeona kuwa watu kuaacha kuchangamana, pamoja na kupiga marufuku kwa mikusanyiko ya watu wengi kumechukua muda mrefu kufanyika na tunaamini kuwa hayo yanaweza kuwa ni moja ya mabo yaliyopelekea ongezeko la kasi la wagonjwa wa corona," ameeleza Dkt Moeti katika mkutano na wanahabari.

Tanzania kwa mara ya kwanza iliripoti mgonjwa wa kwanza wa corona Machi 16 na kufikia sasa idadi ya maambukizi imefikia 284.

Baada tu ya kuripotiwa kwa ugonjwa huo, serikali ya Tanzania ilitangaza kufungwa kwa shule na vyuo vikuu pamoja na matukio ya kukusanya watu wengi kama ligi za michezo ikiwemo mpira na matamasha ya muziki.

Hata hivyo, serikali ya rais John Pombe Magufuli imekosolea vikali kwa kutochukua hatua kali kama kufunga (lockdown) vitovu vya maambukizi kama miji ya Dar es Salaam na Zanzibar.

Jumatano, rais wa Tanzania John Pombe Magufuli liweka wazi kuwa serikali yake haitalifungia jiji la Dar es Salaam.

Licha ya Dar es Salaam kuwa kitovu cha maambukizi, Magufuli amesema jiji hilo la watu milioni sita ndio moyo wa mapato ya Tanzania.

"Wapo wengine wanatoa mawazo ya kuifunga Dar es Salaam, hili haliwezekani. Dar es salam ndio centre (sehemu) pekee ambapo collection (makusanyo) ya revenue (mapato) inapatikana kwa nchi yetu...Zaidi ya asilimia 80 ya mapato yanakusanywa Dar es Salaam," alisema Magufuli alipokutana na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo Jumatano.

Pia alisisitiza kuwa kutokana na wingi wa wakaazi wake, ilikuwa ni jambo la kutegemewa kitakwimu kwa jiji hilo kuwa na wagonjwa wengi zaidi.