Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:25 pm

NEWS: WEMASEPETU ATUPWA GEREZANI SIKU 7 NA MAHAKAMA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imemuamuru Staa Muigizaji wa Bongo Move na Miss Tanzania(2006) Wema Abraham Sepetu kwenda gerezani siku 7 wakati akisubiria uamuzi wa mahakama wa kumfutia dhamana.

Image result for wema sepetu mahakamani

Mahakama hiyo siku ya June 11, 2019 ilitoka hati ya kumkamatwa kwa staa huyo wa Bongo Move, baada ya kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa na mahakama hiyo.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo,Maira Kasonde baada ya mshtakiwa kushindwa kufika mahakama kusikiliza kesi inayomkabili kwa mara nyingine tena.

Novemba 1, mwaka jana Wema alipandishwa katika mahakama hiyo akikabiliwa na shtaka la kusambaza video ya ngono kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, kesi yenye jalada namba KJN/ RB/13607/2018-KUCHAPISHA NA KUSAMBAZA MAUDHUI YA NGONO MTANDAONI na aliachiwa kwa dhamana ya Sh. milioni 10 kupitia kwa Salim Limu.

Shtaka linalomkabili Wema kwa mujibu wa sheria adhabu yake ni kulipa faini isiyopungua Sh20milioni ama kifungo kisichopungua miaka saba.