- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WEMA SEPETU AACHIWA HURU NA KUKAMATWA TENA
Msanii wa Bongo Move nchini Wema Abraham Sepetu amezua taharuki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kugoma kukamatwa na polisi mara baada ya muda mchache mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kumwachia huru na kisha kumkamata tena na kumuweka mahabusu ya mahakama hiyo.
Wakati askari wakimkamata kwa nguvu, Wema aligoma kukamatwa hali iliyosababisha mvutano kwa muda kati askari na mawakili wake, Albert Msando na Reuben Simwanza.
Hata hivyo, askari hao walifanikiwa kumkamata msanii huyo aliyetoka Mahabusu ya Gereza la Segerea Juni 24, mwaka huu ambapo alifika mahakamani asubuhi kwa ajili ya kusikiliza kesi yake inayoendelea mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.
Wakili wa Serikali, Glory Mwenda alidai hana shahidi baada ya shahidi aliyemuandaa, Koplo Safi kudai ni mgonjwa.
Hoja hiyo ilipingwa na Wakili wa Wema, Albert Msando kwa madai kwamba haina mashiko, mahakama ilishatoa ahirisho la mwisho hivyo hawawezi kuahirisha tena.
“Mheshimiwa shauri lipo zaidi ya siku 60, upande wa mashtaka wameshindwa kuleta mashahidi, tunaomba chini ya kifungu namba 225(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 mshtakiwa aachiwe huru,” alidai.
Wakili Mwenda alipinga akidai sheria ya siku 60 inatumika pale tu ambapo upelelezi haujakamilika hivyo aliomba kesi iahirishwe.
Hakimu Kasonde alisema anakubaliana na maombi ya upande wa utetezi, sheria hiyo inatumika wakati wowote hivyo mahakama inamuachia huru mshtakiwa.
Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani.