Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 6:53 am

News: Waziri wa nishati na madini amewata wazanzibar kuwa wavumilivu mpaka mafuta na gesi yatakapopatikana.

Dodoma: WAZIRI wa Nidshati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amewataka Wazanzibar wanaotaka kuendeleza mjadala kuhusu mafuta na gesi yanayoweza kupatikana visiwani humo wasibiri yaonekane.
Amesema kwa sasa utafiti kuhusu nishati hiyo unaendelea hivyo ni vyema kusubiri ili kuwa na uhakika juu ya kile wanachotaka kuendelea kukijadili.

Mbali na hilo imeemelezwa endapo nishati hiyo itapatikana katika eneo la ukanda wa kimataifa zipo sheria za kimataifa zitakazotumika kupata tafsri mbalimbali juu ya namna ya kunufaika nayo.

Profesa Muhongo ame`sema hayo jana jioni wakati wa kuhitimisha mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Amesema sivyema kwa sasa kutaka kuibua upya mjadala kuhusu mafuta na gesi kwa kuwa bado haijafahamika kama yapo na kama kweli yapo kwenye eneo la Zanzibar.

“Tusubiri kwanza yapatikane na tuwe na uhakika yapo eneo gani kisha tuendelee na mjadala huuu.

“Kwa kuwa Zanzibar inapakana na nchijarani ya Kenya na Tanzania Bara yawezekana mafuta hayo yakabainika nje nje ya eneo la visiwa hivyo na kuufanya mjadala huo kutokuwa na mantiki,”amesema

Kauli ya Muhongo ilitokana na hoja iliyoibuliwa na Mbunge Ahmed Nwale aliyedai sheria kuhusu kuliutoa jambo la mafuta kwenye mambo ya muungano ilikiuka katiba ya Tanzania hivyo kutaka mchakato kuhusu suala hilo utaszamwe upya.


Ngwale amedai kwa sheria ya sasa Zanzibar bado haijapewa uwezo wa kumiliki mafuta yake kwa kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) bado inao uwezo wa kuinbgilia kati hususan utakapofika wakati wa kugawa vitalu vya uchimbaji.


Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema SMT haiwezi kuepukwa hususan linapokuja suala la uwakilishi wa kimataifa kwa kuwa nje ya Tanzania mambo yote yanachukuliwa ni ya nchi moja.


“Nje ya Tanzania hakuna jambo hili ni la ,muungano na hili si la muungano, mambo yote yanatazamwa katika sura moja ya Tanzania.


“Hata hivyo Tanzania inao utaratibu wake wa kuwasilisha mambo yake na kuyatetea kwa faida ya nchi kama vile inavyofanyika kwenye mambo mengine yanayohusisha Zanzibar na Tanzania bara,”amesema.


Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju alikanusha kukiukwa kwa katiba ya nchi katika kuliondoa suala hilo kwenye mambo ya muungano.