Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:34 am

NEWS: WAZIRI WA MAREKANI JOHN KERRY AWAPONGEZA WAKENYA KWA KUPIGA KURA

Nairobi: Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje chini Marekani John Kerry amesema kuwa Jumatano ya jana (8.8.2017) mistari mirefu ambayo ameiona katika vituo vya kupiga kura ni ishara ya ahadi ya wananchi kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.

Kerry na aliyekuwa waziri mkuu wa Senegal Aminata Toure na Viongozi pacha wa Kituo cha Carter Center cha usimamizi wa uchaguzi walitembea shule ya Sekondari ya Jamhuri Jijini Nairobi kujionea shughuli ya upigaji kura.


“Ni mapema sana kwetu kutoa majumuisho ya aina yoyote kuhusu uchaguzi, kwa hiyo hatutofanya hivyo, lakini kutokana na yale yaliotokea huko nyuma na kufuatia hatari za siku za usoni, huu ni uchaguzi muhimu sana na wananchi wa Kenya bila shaka wanauchukulia uchaguzi huu kwa makini sana,” amesema Kerry.

Tume ya uchaguzi Kenya inatumia mifumo ya biometric katika kutambua wapiga kura na pia upeperushaji wa kura kielektroniki katika zeozi zima la uchaguzi.