Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 4:13 am

NEWS: WAZIRI WA KILIMO AFUTA VYAMA 3,348 HEWA VYA USHIRIKA

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Japhet Hasunga amevifuta vyama vya ushirika 3, 348 kutokana na kuvibaini kuwa ni vyama hewa baada ya kutofanya kazi kwa muda mrefu.

Waziri amesema kuwa vyama hivyo vimebainika kutotekeleza majukumu yake ya msingi na kusema utaratibu wa serikali kuvifuta vyama hewa utakuwa endelevu kwa vile vitakavyoshindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Akitoa taarifa kuhusu mwenendo wa vyama vya ushirika nchini, Waziri Hasunga amesema uamuzi huo unatokana na kusudio la serikali alilotangaza Januari tano mwaka huu la kutaka kuvifuta vyama hivyo ambavyo vilikuwa havifanyi kazi ama kutotekeleza majukumu yake na vile hewa.

Katika hatua nyingine Mhe.Hasunga amewaonya wafanyabishara kutoka nje ya nchi ambao wanaanza kunyemelea mazao kwa wakulima katika maeneo mbalimbali nchini na amewaagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula kuhakikisha msimu wa mavuno kununua mazao yatakayosaidia kuwa na akiba ya hifadhi ya chakula.