Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:45 pm

NEWS: WAZIRI WA KIKWETE AKIRI KUWEPO KWA TISHIO LA USALAMA TANZANIA

Washington: Waziri wa zamani wa Maliasili na utalii na mbunge wa zamani wa bukoba mjini Khamis Juma Suedi Kagasheki amesema kuwa kwa sasa nchini Tanzania niwazi usalama wa raia upo hatarini, akiandika kwenye ukurasa wake wa twitter Kagasheki amesema kuwa jana baada ya kuwasikiliza vizuri spika wa bunge Job Ndugai na Waziri mkuu Kassim Majali wakati wa kuhairishwa kwa bunge walionesha kuwepo kwa tatizo la usalama wa watu nchini ''Baada ya kuwasikiliza PM na spika katika kuhairisha Bunge, ni wazi lipo tatizo la usalama wa raia nchini, hii si agenda nzuri kwa serekali" aliongea Kagasheki.

Spika wa bunge Job Ndugai aliwatahadharisha wabunge kuchukua tahadhari ya kutotembea hovyo na kukaa kwenye mabaa mpaka usiku wa manane na badala yake warudi mapema majumbani kwao kulea familia hii ni kutokana na kushamiri kwa matukio yanayo tishia usalama wa raia na mali zake, hasa matukio ya hivi karibuni ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kushambuliwa kwa Risasi na watu wasiojulikana Nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, Tukio Lingine ni kuchomwa moto kwa ofisi za wanasheria wa IMMMA Advocates zilizopo upanga jijini Dar es salaam.

Kumekuwepo na sintofahamu kwa wananchi na wanasiasa Juu ya hatua zinazo chukuliwa na vyombo vya usalama katika kushughulikia matukio haya ambapo mpaka ilipelekea baadhi ya wananchi wakiwemo wanasiasa kutaka kuitisha uchunguzi wa kimataifa juu ya matukio ya kiusalama nchini