- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI WA HABARI: REDIO ZA KIJAMII ZISITEKWE NA SIASA
DODOMA: REDIO za Kijamii zimetakiwa kutotekwa na siasa ili kuweze kuepusha mifarakano kwenye jamii. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na michezo Anastazia Wambura wakati akifungua mafunzo kuhusu wajibu wa redio za jamii kwa maendeleo vijijini, namna ya kuhakikisha upatikanaji wa habari, taarifa, fedha na huduma muhimu kwa maendeleo ya Redio.
Amesema redio hizo zinatakiwa kujikita zaidi katika kuangalia masuala ya msingi yanayohusu jamii. "Redio hizi zisitekwe na siasa ili kujiepusha na mifarakano na jamii" alisemaPia alisema moja kati ya changamoto zinazochelewesha ufikiwaji wa malengo hayo ni pamoja na kukosekana kwa nyenzo za kuwafikishia taarifa wananchi.
Amesema wananchi wengi hasa vijijini hawapati taarifa muhimu zinazohusu maendeleo yao, ikiwemo taarifa za kilimo, afya, mazingira,haki za binadamu."Redio za jamii miongoni mwa teknolojia zinazochangia kwa kiasi kikubwa kufikisha taarifa kwa wananchi wengi wa vijijini na kwaharaka" amesema
Amesema takwimu zinaonesha kuwa watanzania wengi wanasikiliza redio ambapo utafiti wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Wilayani Bunda na Bukoba vijijini mwaka 2013 zaidi ya asilimia 80 yawananchi waliohojiwa wanasikiliza au wamiliki wa redio.Wambura alisema pamoja na kiasi hicho kikubwa swali kubwa ni jinsi gani redio zinaweza kutumiwa kuboresha maisha ya wananchi na hatimaye kupunguza umaskini wa kipato.
Amesema katika kutatua changamoto mbalimbali, ESRF kwa msaada wa serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP) waliamua kufadhili kuanzishwa kwa baadhi ya redio za kijamii na kuwapati wananchi fursa ya kupata taarifa muhimu na hatimaye kuinua kipato chao.
Amesema changamotoedio za kijamii ni pamoja na upatikanaji wa habari na taarifa endelevu na zinazolingana na mahitaji ya jamii husika,uhaba wa raslimali fedha za kuendesha redio husika na udhaifu katika usimamizi stahiki wa taasisi hizo. Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk Tausi Mbaga Kida alisema mwaka 2014 ESRF chini ya ufadhili wa shirika la UNDP kupitiamradi wa Capacity Development for Result Based Monitoring and Auditing (CDRBM) ilifanta utafiti katika wilaya sita za Ileje,, Nyasa, Bunda Bukoba vijijini, Ikungi na Sengerema.
"Utafiti huo ulionesha redio ni njia bora zaidi ya upashanaji habari vijijini kwa vule inawafikia watu engi zaidi ukilinganisha na njianyingine za upashanaji habari kama barua pepe, luninga, tovuti, simuza mikononi na magazeti." amesema
Amesema baada ya kuliona hilo utafiti ulipendekeza kuanzishwa kwa redio jamii katika maeneo ya utafiti ili kuwafikishia taarifambalimbali za kuelimisha wananchi ambazo zitakuwa chachu kubwa kwa maendeleo ya sehemu zao.
Amesema ESRF kwa ufadhili wa UNDP ilisimamia uanzishwaji wa redio jamii tatu, Ileje FM, Unyanja FM, Kagera Community Redio na Bunda FM ambapo pamoja na uanzishwaji wa redio hizo redio nyingine mbili Mazingira FM na Sengerema FM zilipata misaada mbalimbali kwa ajili yakujiendesha.