- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI WA FEDHA WA KENYA AKAMATWA NA POLISI KWA RUSHWA
Waziri wa Fedha wa Kenya Henry Rotich na viongozi kadhaa wa wizara ya fedha wamekamatwa Jumatatu ya leo (Julai 22) kwa madai ya rushwa, udanganyifu na Ufisadi kuhusiana na mradi wa ujenzi wa mabwawa mawili wenye thamani ya dola milioni mbili.
"Watuhumiwa wanazuiliwa na wanasubiri kupelekwa mahakamani," mkuu wa polisi ya Kenya George Kinoti ameliambia shirika la Habari la AFP, akiongeza kuwa watuhumiwa hao wamejisalimisha kwa maafisa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya umma, Noordin Haji, kuomba hapo awali waweze kukamatwa.
"Henry Rotich anatuhumiwa kukiuka muongozo wa utoaji wa kandarasi iliopewa kampuni ya Italia CMC de Ravenna yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 450 kwa ujenzi wa mabwawa mawili nchini, " imesema taarifa kutoka ofisi ya mkurugenzi wa Mashitaka ya umma.
Noordin Haji ameeleza kwamba watashtakiwa kwa "kupanga kufanya udanganyifu, kushindwa kutii muongozo unaotumika katika upatikanaji wa kandarasi" miongoni mwa mambo mengine.
"Katiba yetu inasisitiza baadhi ya maadili yetu yakiwemo uadilifu… kuyatimiza hususan kwa walio uongozini, " ameongeza Mkurugenzi wa Mashitaka ya umma.
Maafisa wengine walioagizwa kukamatwa na kushtakiwa ni pamoja na katibu mkuu katika wizara ya fedha Kamau Thugge, Dkt Susan Jemutai Koech kutoka wizara ya jumuiya ya Afrika mashariki na mkurugenzi msimamizi wa mamlaka ya maendeleo ya Kerio Valley (KVDA) David Kimosop.