- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI WA AFYA ATAKA HATUA KALI ZICHULIWE KWA WANAOZUSHA TAARIFA KUHUSU UGONJWA WA EBOLA.
DODOMA: Waziri wa Afya maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watu ambao wanasambaza tarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna ugojwa wa Ebola nchini.
Waziri Ummy ametoa onyo hilo wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa taifa wa usalama wa afya ambao utasaidia taifa kuweka mifumo mizuri ya kujiandaa na maafa kama ugonjwa wa ebola.
Waziri wa Afya Zanzibar Mahamoud Thabiti Kombo amesema mpango huo utasaidia kulinda mipaka ya nchi ili kuepuka magonjwa ya milipuko kwa wageni wanaoingia nchini.
Kupitia mpango huo wa taifa wa usalama wa afya naibu waziri wa nchi ofisi ya rais TAMISEMI Seleman Jaffo akatoa maagizo kwa wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya na wakurunzi.
Imeelezwa kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza Duniani kuzindua mpango huu ambao utajenga uwezo wa kugundua,kuzuia na kuchukua hatua za kukabilianamatukio hatarishi ya kiafyana magonjwa ya mlipuko.