- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI WA AFYA ASISITIZA UBORA WA BIDHAA KATIKA KIWANDA KIPYA CHA DAWA NA VIFAA TIBA SIMIYU
DODOMA: Bodi ya wakurugenzi wa kiwanda cha vifaa tiba cha Simiyu(SIMIYU MEDICAL PRODUCTS) wametakiwa kuzalisha bidhaa zenye viwango na kukidhi mahitaji ya ndani nan je ya nchi.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa bodi ya wakurugenzi wa kiwanda hicho uliofanyika leo jijini hapa.
Waziri Ummy amesema kuwa bidhaa zenye viwango itasaidia kuuza nje ya nchi na watanzania kuzitumia kwani lengo la serikali ya awamu ya tano ni ya kukuza uchumi wa viwanda
“Lakini mhakikishe maamuzi yeyote mtakayofanya mjiridhishe je ni kwa ajili ya maslahi ya Taifa na je yatatufikisha kule tunapotaka kufika,jiridhisheni katika kuhakikisha mnatumia fedha hizi chache tulizonazo katika kuleta matokeo ya haraka haya ndiyo ya kuyazingatia”.Alisisitiza Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy aliitaka bodi hiyo kuhakikisha wanaongeza thamani ya mazao ya nchi kwa kuzalisha bidhaa nchini na kuondokana na uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi,kuongeza ajira na hata kuondokana na uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.
Hata hivyo aliwataka wasiangalie bidhaa zinazotakana na pamba hivyo kwa baadae ni bora wakaangalia bidhaa zingine zinazohitajika ambazo zinanunuliwa kwa haraka sana kutoka MSD kwani bohari ya Dawa hivi sasa imepata mkataba wa kununua bidhaa za hospitali kwa niaba ya nchi kumi na sita za nchi ya SADC hivyo wahakikishe bidhaa zinazozalishwa zina viwango na ubora na uzalishaji unakidhi soko la ndani nan je ya Tanzania.
Katika hatua nyingine Waziri Ummy amempongeza Mtanzania Dkt. Aswar Hilonga kwa kutunukiwa tunzo na Shirika la Afya Duniani kutokana na Ubunifu wake wa kutengeneza mtambo wa kuchuja na kusafisha maji.
Mtambo huo unaotumia nanotechnology una uwezo wa kuchuja maji na kuyafanya yawe safi na salama kwa matumizi ya binadamu na kuondoa bakteria, kemikali na taka katika maji.
"Asilimia 60 ya wagonjwa wa nje wanaokwenda Hospitalini wanatokana na kiwango duni cha hali ya usafi ikiwenyo unywaji wa maji yasiyo safi na salama. Hivyo kupitia teknolojia hii tunaweza kuokoa fedha za Serikali kwa ajili ya kutibu wagonjwa" amesema Waziri Ummy.
Kwa upande wake Dkt. Hilonga ameiomba Serikali kuweza kuunganisha mtambo huo wa maji ambao unauzwa kwa bei nafuu katika Taasisi za Umma ambao unachuja maji kwa kuondoa batkeria na kemikali na taka katika maji ndani ya muda mfupi.