Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 12:05 pm

NEWS: WAZIRI WA AFYA 55% YA WATANZANIA WANATUMIA VYOO DUNI

Dodoma: Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe. Ummy Ally Mwalimu amewataka wadau wa masuala ya usafi wa mazingira wapitishe kampeni moja ya mazingira iitwayo NIPO TAYARI Ambayo itasaidi kuongeza kasi ya uboreshwaji hali ya usafi nchini.

Ummy ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Nembo Mpya ya kampeni ya usafi wa mazingira NIPO TAYARI Katika Hotel ya Morena mjini Dodomaamesema kama wadau wa maendeleo tuungane kwa pamoja ili kutoa elimu kwa wananchi kuwasaidia kujua usafi wa mazingira ikiwemo matumizi ya vyoo na ubora na kusaidia sehemu za wazi husababisha magonjwa na vifo vitokanavyo na uchafu kama vile kipindupindu, kuhara damu ,minyoo na nimonia hali duni.

‘’Naomba kila mmoja wenu ashiriki kwenye jitihada za serikali kuhakikisha tunafanikisha swala la usafi wa mazingira ,’’amesema Ummy

Kujisaidia ovyo hovyo imekua ni tatizo kubwa kwa zaidi ya miaka 25 sasa na kulingana na ripoti ya mwaka 1990 inaonseha10% Ya watu waishio vijijini hawakua na na vyoo, 13% Kwa mwaka 2000, 16% kwa mwaka 2011 . Zaidi ya 55% ya watanzania wanatumia vyoo duni vyenye madhara ya kiafya na kiuchumi.

Ummy amesema hata hivyo kulingana na ripoti ya Benki ya Dunia inaonyesha kuwaTanzania inapoteza 1% ya pato la ndani la taifa kutokana na hali duni ya usafi wa mazingira ameongeza kuwa kiasi hiki ni kikubwa sana kwa mataifala kuhudumia watoto [UNICEF] inaonesha dunia kupoteza watoto milioni 1.7 kila mwaka kutokana na magonjwa ya kuhara na nemonia.