Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 1:21 pm

NEWS: WAZIRI UMMY AWATAKA MAAFISA MAENDELEO KUFUATILIA TAKWIMU.

DODOMA: Maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya mkoa na halmashauri kote nchini Wametakiwa kufuatilia na kuwa na takwimu za wahanga wa matendo ya ukatili badala ya kuliachia jeshi la polisi.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto UMMY MWALIMU Ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano mkuu wa wataalam wa maendeleo ya jamii.

Pia amewataka wataalam hao kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kuwa na takwimu hizo na kwamba alishailekeza wizara kushughulikia suala hilo baada ya marekebisho ya sheria ya elimu mwaka 2018 inayopendekeza wakuu wa shule kutoa taarifa za wanafunzi waliokatiza masomo kwa kila robo mwaka lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika.

Aidha waziri Ummy amekemea tabia ya baadhi ya wataalam wa idara ya Afya kuingilia majukumu ya wataalam wa idara ya maendeleo ya jamii na kuwataka waache mara moja.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi idara ya maendeleo ya Jamii Wizara hiyo Patrick Golwike amesema miongoni mwa mada zitakazowasilishwa katika kongamano hilo ni pamoja na Serikali kuhakikisha inafikia hatua ya kujali mahitaji ya mmoja mmoja,nafasi ya maendeleo ya jamii katika kuchochea maendeleo,Teknolojia ya habari na mawasiliano inavyoweza kufanikisha kazi za maendeleo ya jamii,kutawala hisia wakati wa majukumu ya maendeleo ya jamii na matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika kufanikisha maendeleo endelevu.

Akiendelea kuelezea amesema‘’ Mchango wa wananachi katika kufikia uchumi wa wakati kwa kutumia teknolojia rahisi na za kisasa,matumizi ya teknolojia katika utatuzi wa changamoto wa mila na desturi, zenye kuleta madhara, Ushiriki wa Wanaume kama wakala wa mabadiliko wa kuzuia ukatili wa kijinsia,CHF iliyoboreshwa na utekelezaji wa program ya lishe na kuongeza kuwa mwisho wa kongamano hilo watatoka na adhimio litakalosaidia kuboresha utendaji wa wataalamu kutoka srikali hata Sekta binafsi,’’

Mkutano huu unaambatana na kongamano la wataalam wa maendeleo ya jamii kutoka sekta ya umma, binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, taasisi na vyuo vya maendeleo ya jamii.