Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:58 am

NEWS: WAZIRI UMMY APANGA MIKAKATI NA WATAALUM WA AFYA KUDHIBITI CORONA

Dar es Salaam. Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amekutana na wataalam wa afya nchini humo na kujadili hali ya mwenendo wa kudhibiti ugonjwa wa corona nchini Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya leo Ijumaa Machi 20, 2020 imesema kuwa katika kikao hicho cha Waziri Ummy na wataalamu hao wa afya wamejadili mambo manne.

Jambo la kwanza lililojadiliwa kwenye kikao hicho ni kuhakikisha hospitali zote za Serikali na binafsi zinazingatia miongozo ya Wizara kuhusu magonjwa ya mlipuko kabla ya kuwahamisha wagonjwa kwenye hospitali za rufaa za Serikali.

Jambo la pili lililojadiliwa kwenye kikao hicho ni kuitaka Serikali kuendelea kutoa elimu na maelezo sahihi kwa wananchi kuhusu jinsi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona, dalili zakje na hali halisi ya mweenendo wa ugonjwa huo nchini.

Suala lingine ambalo kikao hicho kimejadili ni kuvishauri vyombao vya habari kutumia waataalam wa afya kutoka wezara ya afya na taasisi zake pamoja na waganga wakuu wa mikioa na halmashauri ili kuhakikisha mnaudhui ya uelimishaji kuhusu ugonjwa huo ni sahihi.

Corona umekuwa ugonjwa hatari duniani, huku ukiwa umeshaambukiza zaidi ya watu 250,000 duniani kote na 637 Barani Afrika.

Nchini Tanzania wizara ya Afya imesharipoti visa vya watu sita wakiwemo watu wawili maarufu(Mwanamuzi wa Bongofleva Hamisi Mwijuma maaarufu kama Mwana FA na Meneja wa mwanamuzi wa Tanzania Diamond Platnumz)

Taarifa hiyo imesema kuwa wagonjwa wote waliothibitika kuwa na maambukizi ya corona wanaendelea na matibabu.

“Hadi kufikia Machi 20, 2020 Tanzania imethibitisha kuwepo kwa kesi 6 za wagonjwa wa corona ambao wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa watumishi wa sekta ya afya” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa Wizara ya Afya inaendeleaa kutoa huduma ya afya kwa watu waliothibitika kuwa na ugonjwa wa corona na kudhibiti maambukizi mapya ya ugonjwa huo.