- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI TIZEBA: ''WATAKAO UNZA MBOLEA KWA AMBAYO SIYO ELEKEZI WAKAMATWE''
DODOMA: Waziri Wa kilimo mifungo na uvivu Dkt.Charles Tizeba amewataka wakulima nchini kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi kama wataunziwa mbolea kwa bei ambayo siyo elekezi kwa maduka ya pembejeo.
Akizungumza na waandishi Wa Habari Leo mjini Dodoma Waziri Tizeba amesema aina ya mbolea hizo ni mbolea za kupandia(DAP) na ya kukuzia (Urea).
Tibeza amesema matumizi ya mbolea yamefikia wastani Wa kilo 19 za virutubisho kwa hekta moja.
"Kwa mujibu wa ibara ya 56 ya kanuni za mbolea (2011)na marekebisho yake ya mwaka 2017 ( the fertilizer (amendment) regulations,2017) na kuchapishwa katika gazeti La serikali (GN) na.50la February 17,2017, mbolea aina zote zinatakiwa kuuzwa kwa bei iliyopangwa na mamlaka ya uthibiti Wa mbolea Tanzania (TFRA) iliyo chini ya wizara ya kilimo mifungo na uvivu''.amesema
Hata hivyo Waziri huyo amesema bei elekezi ya mbolea iliyotangazwa had I kwenye maduka ya rejareja ni mfuko Wa kilo 50 Wa mbolea ya kupandia (DAP) ni tshs. 50,500 sawa na 53,000 kwa mikoa ya kanda ya mashariki, kati na kaskazini aidha kwa mikoa ya kanda ya magharibi,ziwa na nyanda za juu kusini bei elekezi ya mfuko mmoja Wa mbolea Wa kilo 50 utakuwa kati ya tshs 53,500 na 56,000.
Ameongeza kuwa bei hizi ni pungufu kwa asilimia 13 hadi 42 ukilinganisha na bei ya mbolea aina ya DAP iliyokuwa ikiuzwa kati tshs 41,000 na 43,000 na katika mikoa ya kanda ya mashariki kati na kaskazini ,bei itakuwa kati ya tshs 38,000 na 43,000 bei hizi ni pungufu kwa wastani Wa asilimia 15 ukilinganisha na bei ya mbolea ya haina UREA ilkyokuwa ikiuzwa kati ya tshs 45,000 na 70,000 kwa mfuko Wa kilo 50 ( kiambatanisho Na 1). bei hizo zilianza kutumika kuanzia agosti 16 mwaka huu.
Sanjari na hayo Waziri ametoa wito kwa wataalam na wadau Wa kilimo kutoa ushirikiano Wa dhati katika kuwaelekeza wakulima matumizi sahihi ya mbolea ili kufikia lengo La kujitosheleza kwa Chakula kwa taiga sambamba na kuongeza gharama za mbolea.