November 26, 2024, 5:48 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI SIMBACHAWENE AWAMWAGIA SIFA NEMC
DAR: Waziri wa Nchi, Ofi si ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, George Simbachawene amepongeza utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na kulitaka kuendelea kusimamia sheria na taratibu katika kutekeleza majukumu yake ili kufi kia malengo ya taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo na kuzungumza na menejimenti ya NEMC jijini Dar es Salaam , Simbachawene alisema mbali ya kuridhishwa na kazi za baraza anategemea kupata ushirikiano mkubwa.
"Nahitaji ushirikiano wenu ili niweze kufanikisha majukumu niliyokabidhiwa na Rais John Magufuli ya kusimamia mazingira hapa nchini,” alisema Simbachawene ambaye aliambatana na naibu wake waziri, Musa Sima.
"Matumaini yangu kwa baraza ni makubwa kutokana na hali na utayari wa watendaji wake katika kutekeleza majukumu yao na kuifanya nchi kubaki katika hali ya mazingira endelevu.
Alisema jukumu la kutunza mazingira ni la kila Mtanzania, hivyo akalitaka baraza hilo kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi umuhimu wa mazingira na athari zake endapo tahadhari hazitachukuliwa.
"Mimi bado mgeni katika wizara hii hivyo nategemea kujifunza zaidi kutoka kwenu watendaji wa baraza hivyo ushirikiano wenu kwangu ndio utaniwezesha kuelewa kwa haraka mambo yote yanayofanywa ili twende sambamba katika utekelezaji wa majukumu," alisema.
Waziri huyo alisema ana uzoefu wa muda mrefu katika uongozi lakini wizara aliyopewa ni mpya kwake na ina changamoto nyingi kutokana na umuhimu wa utunzaji wa mazingira kutokana na kuongezeka shughuli za kibinadamu hivyo kuna kila sababu ya kujifunza zaidi ili kuweza kusimamia kikamilifu mazingira yawe salama kwa kizazi cha sasa na baadaye.
Aidha, Simbachawene alielezwa changamoto za kiutendaji za baraza na kuagiza waziainishe na kuwasilisha wizarani ili zipatiwe ufumbuziliweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
"Kumekuwa na lawama nyingi za kiutendaji katika kutoa vyeti vya tathmini ya athari ya mazingira kwa wawekezaji, hivyo kwa kuwasilisha changamoto zetu wizarani na kufanyiwa kazi nina uhakika hazitakuwapo tena na kutachochea ongezeko la wawekezaji,"alisema.
Simbachawene aliitaka NEMC iende sambamba na azma ya serikali ya kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025 na kumtaka kila mtumishi katika eneo lake kuondoa vikwazo, upungufu na changamoto zilizopo. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka, mbali ya kumpongeza Simbachawene kwa kuteuliwa kwake, alimuahidi kumpa ushirikiano ili aweze kufikia malengo aliyojiwekea.