Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 4:15 pm

NEWS: WAZIRI SHONZA AMUOMBA RADHI RAIS MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA MPINZANI

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini, Juliana Shonza amewaombea radhi wananchi wa jimbo la Momba kwa kitendo cha kuchagua mbunge ambaye hatokani na chama chake yaani CCM na badala yake wakamchagua kutoka upande wa upinzani.

Kama unakumbukumbu Mbunge wa jimbo la Momba ni David Silinde wa Chadema.

Shonza ameomba msamaha huo mbele ya Rais John Magufuli aliyekuwa njiani kutoka mkoa wa Songwe kwenda Katavi akiahidi kosa hilo halitafanyika tena mwaka 2020 kwa kuwa upinzani hautapewa nafasi.

“Nachukua nafasi hii kuomba radhi kwa niaba ya wananchi, tunaahidi hatutarudia makosa, upinzani hautakuwa na nafasi katika mkoa wa Songwe kuanzia viongozi wa chini hadi juu kote itakuwa kijani,” amesema Shonza.

Kwa upande wake, Rais Magufuli amewataka wakazi wa jimbo hilo kuwalaumu viongozi wao kwa kushindwa kutatua kero ya uhaba wa maji.

“Kukosekana kwa maji hapa mimi sio wa kulaumiwa, ningejuaje kama mna shida ya maji kama mbunge au diwani wenu hajanipa taarifa? Kama mnaona viongozi wenu mliowachagua hawafanyi kazi vizuri watoeni.”

“Mimi nawapenda wote lakini kuna watu nawapenda zaidi, mbunge wenu angekuwa sio wa chama cha jirani ningekuwa naye hapa nimuulize maswali kwa nini maji hakuna,” amesema Magufuli.