November 24, 2024, 4:42 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MWIJAGE ATAGAZA VITA KWA WAINGIZAJI WA BIDHAA BANDIA NCHINI
DODOMA: Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ametangaza vita kwa watumishi wanaoruhusu uingizwaji wa bidhaa bandia nchini, na kutoa onyo kwamba watakao fanya hivyo wajiandae kuondoka.
Mwijage ametoa onyo hilo juzi Bungeni mjini Dodoma, wakati akisoma bajeti ya wizara yake, ambapo pia alipiga marufuku bidhaa bandia kuingia nchini kutoka nje ya nchi kuanzia Julai mosi mwaka huu.
“Ikifika mwezi Julai mwaka huu, kama bidhaa feki zikipita kuingia nchini mtakuwa hamnitakii mema, na walio chini yangu mkae kabisa mkao wa kuondoka kama bidhaa zisizokidhi viwango zitapia na kuja kuumiza viwanda vyetu nchini,” alisema.