- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MWAKYEMBE AKEMEA HONGO YA WASANII KWA WATANGAZAJI
DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Habari, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe amekemea tabia ya baadhi ya waandishi wa habari kuchukua pesa (mshiko), ili wapige redioni nyimbo za wasanii,
Alisema hatakubali tabia hiyo iendelee na kwamba vyombo vya habari vinatakiwa kulipa pesa ili vipige nyimbo za wasanii redioni na kuzionesha katika Luninga.
Mwakyembe aliyasema hayo jana katika ukumbi wa Vijana uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na Chama cha Wasanii wa Muziki wa Dansi Nchini (CHAMUDATA).
“Ni upendeleo tu, baadhi ya wasanii ndiyo wanasikika wengine wanazimwa kabisa haiwezekani kabisa wasanii wenyewe wanakufa wakiwa maskini na majina makubwa harafu kuna wengine wanabadilisha magari kila wiki,” alisema.
Aidha alisema kuwa atahakikisha wasanii wananufaika na kazi zao na amewataka kuwa na mshikamano katika kupigania haki katika sanaa ya muziki ikiwemo kuwa na mikataba kati ya mmiliki wa bendi.
“Nimeelezwa kuwa kuna watu wengine hawataki mikataba, hapana ni lazima walazimishwe, twende kwenye ngazi tofauti kabisa ya mahusiano kwa sababu bila maandishi tunapoteza vitu vingi sana,” alisema.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Hassan Msumali alisema kutonufaika kwa kazi zao ni changamoto kubwa zinazowakumba huku wakiomba kupewa muda wa ziada kutokana na ukomo wa muda wa saa sita usiku waliowekewa.
“Upigaji wa nyimbo za dansi katika vyombo mbalimbali vya habari hautendi haki kwa mziki wa dansi,” alisema.
Doreen Sinare, OAfisa Mtendaji Mkuu COSOTA alisema elimu inahitajika kwa wasanii kwa kuwa wengi wao hawajui utofauti kati ya hatimiliki na hakishiriki na kuwa changamoto kubwa katika muziki wa dansi zinatokana na kutokuwa na mikataba.
#Mwanahalisi.