- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MPINA ATEKETEZA TANI 11 ZA SAMAKI AINA YA SATO
Waziri wa mifugo na uvuvi hapa nchini, Luhaga Mpina leo Machi 12 amefanikiwa kuteketeza Tani 11 za samaki aina ya Sato baada ya kubainika kuwa wana vimelea vya sumu.Samaki hao ambao wanaripotiwa kuingizwa nchini kwa njia za panya kutoka nchini China wana thamani ya dola za Marekani 33,000.
Mpina amesema watu walioingiza samaki hao nchini walitumia njia zisizo halali.
Samaki hao walitelekezwa baada ya mamlaka kukamata shehena hiyo, Kama ilivyo ada samaki hao walipitia kwenye vipimo kabla ya kuamuliwa kupigwa mnada, ndipo walipobaini kuwa samaki hao wana kiwango kikubwa cha kemikali ya Zebaki ambacho ni hatari kwa matumizi ya binaadamu.
Aina nyingine ya sumu iliyopatikana kwenye samaki ni viatilifu vya DDT.
Mamlaka zimetahadharisha watu kutofanya biashara kinyume cha taratibu kuepuka kufilisiwa na upoteza mitaji yao,
Mpina amesema kuwa Kutokuwepo kwa nyaraka zinazo onyesha kama samaki wameidhinishwa kuingia nchini kutoka kwa mamlaka ya nchi walikotoka ndio kilichowapa hofu kubwa pia Nyaraka kuonyesha kuwa wamezalishwa au kuvuliwa kwa njia halali huko walikotoka.