- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MPINA APIGA MARUFUKU MACHIMBO YA MCHANGA
Pwani: Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina amefunga machimbo ya mchanga katika kijiji cha Kolangwa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa kile serekali inachodai kuwa ni Uharibifu wa mazingira.
Mpina amefanya maamuzi hayo Septemba 21 baada ya kubaini uharibifu wa mazingira unaofanywa na wachimbaji wa mchanga katika machimbo hayo.
Mpina ametoa agizo la kufungwa kwa machimbo hayo akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa mazingira mkoani Pwani ambapo amebaini uharibifu huo umechangiwa na Taasisi za Serikali ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Idara ya Madini na Baraza la Taifa na Usimamizi wa Mazingira NEMC.
Waziri amebaini kuwa uchimbaji huo umefanyika bila wananchi kushirikishwa na haukuzingatia miundombinu na sheria ya Mazingira pia makazi ya watu.
Kufuatia mapungufu hayo, Mpina ameagiza Taasisi hizo za Serikali kufuatilia uharibifu huo uliofanywa kwa muda wa wiki mbili.