Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:38 am

NEWS: WAZIRI MPINA AIAGIZA TAKUKURU KUBAINI UPOTEVU WA BIL 2.6 MAABARA YA UVUVI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ameigiza taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serekali (CAG) kuchunguza upotevu wa fedha wa Shilingi Bilioni 2.6 za Ujenzi wa Maabara ya ya Kisasa ya Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kituo cha Dar es Salaa.

Mpina ametoa agizo hilo Leo Machi 31, 2020 mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) jijini Dar es Salaam, WaziriMpina alisema amebaini mradi unaojengwa miundombinu yake ni midogoikilinganishwa na mkataba ulioridhiwa wash. bilioni 2.6 na kwamba taarifa ya uhakiki ya mradi huo itawasilishwawizarani ikiwa na mapendekezo ya hatua za kuchukua dhidi ya wizi huo wa fedhaza umma.

Hivyo Waziri Mpina ameunda tume ya kiuchunguzi itakayofanya kazi kwa siku saba na kuwahusisha wataalamu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kubaini ukweli wa gharama halisi za mradi huo.

WaziriMpina alisema thamani halisi ya mradi huo hailingani na fedha zilizotolewa na
Serikali huku akitolea mfano baadhi ya miradi ya ujenzi wa majengo mbalimbali
ikiwemo vituo vya afya na hospitali za wilaya zinazojengwa maeneo mbalimbali nchini.

Hatahivyo wakati wa mjadala ukiendelea wa kuhoji matumizi ya fedha hizo kwenye
mradi huo, mmoja wa wakandarasi wanaojenga majengo hayo alimweleza Waziri Mpina
kuwa hadi mradi utakapomika kutabaki ‘chenji’ kiasi cha shilingi milioni 500
jambo lililotilia mashaka na kuibua maswali mengi juu ya gharama halisi za
mradi huo.

Kufuatia mkanganyiko huo wa maelezo yamkandarasi na hali halisi iliyoonekana kwenye mradi huo ndipo Waziri Mpinaakalazimika kutangaza uamuzi huo wa kuundwa tume hiyo ili iweze kufanya tathminiya gharama ya mradi iliyofanywa na Mshauri mwelezi wa mradi, namna zabuni ya
kumpata mkandarasi ilivyotangazwa na namna mshauri mwelekezi alivyopatikana na
hali ya ujenzi unavyoendelea kwa sasa ili kujua dosari ilisababishwa na nani.

Hivyo Waziri Mpina akabainisha kuwa baada ya kazi hiyo ya uhakiki kukamilika ndani ya siku saba ukweli utajulikana na hatua zote zilizopitiwa katika mradi huo ili kubaini kama Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2004 ilikiukwa ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa wote watakaohusika na ubadhirifu huo wa fedha za umma.

“Sikubaliani na hizi gharama za mradi majengona miundombinu ni midogo ikilinganishwa na mkataba wa bilioni 2.6, BOQilihakikiwa na wahandisi wa wizara, washauri waelekezi walijiridhisha kwambaiko sawa na ujenzi ukaenda hadi bilioni 2.6 mtu yeyote akija anakataa” alihoji
Waziri Mpina.

HivyoWaziri Mpina ameagiza ujenzi wa mradi huo uendelee bila kusimama na ukamilike ifikapo Aprili 20 mwaka huu kama mkataba unavyoeleeza na baada ya jengo litazinduliwa ikiwa ni sehemu ya kuleta mageuzi makubwa ya sekta ya uvuvi kupitia eneo hilo muhimu la utafiti.

“Nitaletatimu ya ukaguzi itakayofanya uhakiki wa thamani ya fedha katika ujenzi wa jengo hili, kuanzia kwenye kutangaza tenda yenyewe, thamani ya mradi, kumpata
mkandarasi mwenyewe, cost estimates zilizofanywa na wizara na baadae watafanya
uhakiki wa kinachoendelea kujengwa hapa na kujua thamani halisi inayotakiwa na
kwanini mradi huu upitishwe hadi kusainiwa”alihoji Waziri Mpina.

Menejawa Mradi wa Swiofish, Flora Luhanga alisema mradi huo wa ujenzi wa Jengo la
Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi ulianza Juni 10, 2019 kwa gharama ya
shilingi bilioni 2, 609,491,754 unajengwa na Mkandarasi Kampuni ya Petra
Construction Limited na kusimamiwa na Kampuni ya YP Architect