Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 8:50 pm

NEWS: WAZIRI MPANGO AYASHUKIA MABENKI NA TAASISI ZA FEDHA NCHINI.

DODOMA: Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ameyataka Mabenki na Taasisi za fedha nchini kuangalia upya namna wanavyokokotoa viwango vya riba kwani vinawaumiza wafanyakazi na wajasiriamali wadogowadogo.

Dkt. Mpango ametoa agizo hilo Leo Jijini Dodoma katika zoezi la ugawaji wa hati 203 za viwanja kwa wanachama wa HAZINA SACCOS.

Waziri Mpango amesema kuwa kwa siku za hivi karibuni zimejitokeza Taasisi zinazotoa mikopo yenye riba kubwa kwa wajasiriamali na watumishi wa serikali jambo ambalo yeye kama msimamizi mkuu wa sekta ya fedha nchini hakubaliani nalo.

Pia ameiagiza benki kuu ya Tanzania (BOT) kufanya utafiti juu ya riba zinazotozwa endapo zina sababu za msingi ama zinalenga faida inayomuumiza mteja.

Awali mwenyekiti wa Hazina SACCOS, Aliko Mwaiteleke amesema changamoto zinazowakabili ni pmoja na maeneo mengi waliyoyapima hutwaliwa kwaajili ya ujenzi wa mindombinu ya barabara na Reli.