Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 12:22 am

NEWS: WAZIRI MPANGO ASIFIA SEREKALI KUPUNGUZA MISAADA TOKA NJEE

Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipangowa Tanzania Dk Philip Mpango amesifia kitendo cha Serekali ya awamu ya tano kupunguza misaada kutoka njee, amesema kitendo hicho jambo jema kwake. Waziri Mpango ametoa kauli hiyo leo Jumatano Januari 8, 2020 wakati akipokea gawio kutoka kwa taasisi na mashirika ya umma 13.

Image result for Dk Philip Mpango na waandishi"

Mashirika hayo ni miongoni mwa mashirika yaliyotajwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli Novemba 24, 2019 kwamba wenyeviti wao wasipopeleka gawio, wajitathimini na ikibidi waachie ngazi ifikapo Januari 23, 2020 saa sita usiku.

Waziri Mpango amesema suala la kutegemea misaada kutoka kwa mataifa hayo ambayo wakati mwingine yanatoa mikopo ya masharti magumu, siyo jambo la kujivunia hata kidogo. "Hakuna cha mjomba, lazima tujitegemee sisi wenyewe na moja ya mfano wa kujitegemea ni huu wa kutoa magawio ambayo yanakwenda kusaidia wanyonge," amesema Waziri Mpango.

Waziri huyo aliwataka wenyeviti na wakurugenzi kujitathimini kwani siku zimebaki chache na wakishindwa waondoke wenyewe kwani Tanzania ina watu wengi wenye sifa za kufanya kazi hiyo

Awali, Msajili wa Hazina nchini Tanzania, Athuman Mbuttuka amesema bado mashirika na taasisi 36 ndiyo hawajapeleka gawio kama walivyoagizwa na Rais Magufuli. Mbuttuka amesema hadi sasa kiasi cha Sh20.8 bilioni kimeshatolewa tangu Novemba 24, 2019 na wanaendelea kutoa. Ameyataja mashirika na taasisi hizo 13 ni na kiwango walichotoa kwenye mabano ni; vyuo vikuu Dar es Salaam (Sh1 bilioni), Dodoma (Sh500 milioni), Mzumbe (Sh137 milioni), Muhimbili (Sh110 milioni), Ushirika Moshi (Sh150 milioni) na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Sh100 milioni).

Wengine ni Star Media na NFRA zote zikipeleka Sh500 milioni, PSPTB (Sh350 milioni), TTB (Sh200 milioni), NDC (Sh185 milioni), EPZ wametoa (Sh100 milioni) na Agriculture Input Trust Fund wametoa Sh100 milioni.