Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:35 am

NEWS: WAZIRI MPANGO AITAKA TRA KUONGEZA KASI YA UKUSANYAJI MAPATO

Dodoma: Waziri wa Fedha na Mipango Dokta Philip Mpango ameiyagiza mamlaka ya mapato nchini (TRA) iongeze jitihada zaidi katika ukusanyaji wa mapato ili kukia malengo ya serikali ya ukusanyaji wa kodi ambapo kati ya Julai mpaka Desemba 2018 mamlaka ya mapato nchini ilikusanya mapato ya kodi yaliyokia shilingi trilioni 7.8 ambayo ni sawa na asilimia 88.7 ya makadirio ya kipindi hicho.

Dokta Mpango ametoa kauli hiyo leo Jumapili Januari 20 jijini Dodoma wakati akiongea na baraza la wafanyakazi wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) na kutoa changamoto kwa wafanyakazi hao kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ambapo katika kipindi cha mwaka 2018 kodi ya ushuru wa bidhaa ilikia a silimia 97.1 ya lengo, kodi ya VAT ilifkia asilimia 87 tu ya lengo, huku kodi ya mapato ikikia asilimia 86.4 na kodi ya majengo ilikia asilimi 62 tu na kutaka elimu iyeendee kutolewa zaidi kwa wananchi juu ya umuhimu wa kulipa kodi hiyo ya majengo kote nchini.

Katika hotuba yake Waziri Mpango akawataka wafanyakazi wa mamlaka ya mapato nchini kote nchini kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyonazishwa na seriakali ya awamu ya tano ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa mto Ruji megawati 2100, miradi ya kujenga barabara, miradi ya ujenzi na ununuzi wa meli mpya katika maziwa makuu pamoja na miradi ya afya.

Dokta Mpango amesema dhamira ya kukusanya mapato inapaswa kutekelezwa kwa dhati kutokana na nchi sasa kutotegema wafadhili kwa kuwa kwa sasa hawapo na nchi haitaki misaada yenye masharti.