- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MPANGO AFANYA MAZUNGUMZO NA BOSS WA BENKI YA DUNIA
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) Leo Octoba 16, 2019 amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayewakilisha nchi za Afrika Bi. Anne Namara Kabagambe, Mjini Washington DC, Marekani.Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango,Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mohamed Abdiwawa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Khamis Omary wakiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia(hayupo pichani)kuhusu miradi ya maendeleo Tanzania
Mazungumzo hayo yalilenga katika kubadilishana uzoefu juu ya utekelezaji wa Sera mbalimbali za fedha na namna uchumi wa Dunia unavyoendeshwa.
Katika mazungumzo hayo baadhi ya miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa(SGR), ujenzi wa Bwawa kubwa la kuzalisha umeme la mto Rufiji, mradi wa elimu,na miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), ilijadiliwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kundi la Afrika Bi Anne Namara Kabagambe na Mshauri Mwandamizi kundi la Afrika Bw.Zarau Kibwe akielezea mafanikio aliyoyaona alipotembelea miradi ya Maendeleo Tanzania
Mpango (Mb) ameitaka Benki ya Dunia kujikita zaidi katika kusaidia sekta ya kilimo nchini Tanzania ili kuweza kuwainua kiuchumi wakulima hasa wale wa kati na wadogo.
Dkt.Mpango aliyasema hayo wakati wa kikao cha majadiliano na timu nzima ya Benki ya Dunia ambayo inafanya kazi nchini Tanzania na wengine kutoka Makao Makuu ya Benki hiyo nchini Marekani.
Mhe.Mpango alisema katika mkutano huo walipitia kwa pamoja utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea hivi sasa inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, lakini pia walipitia na kujadili miradi ambayo inaanza kufikiriwa kwa ajili ya utekelezaji kwa mwaka utakaofuata.
‘’Moja ya vitu vilivyonifurahisha mwaka jana kwenye mjadala niliwaaomba sana kwamba hatuwezi kuendelea kuitaka Benki ya Dunia isaidie kwenye miradi mingine tu ni lazima nguvu kubwa ielekezwe pia kwenye miradi ya kilimo ambayo kwa sasa msaada wa Benki ya Dunia katika miradi hiyo ni kidogo sana’’ alisema Dkt.Mpango.
Aidha Dkt.Mpango alielezea dhamira ya Tanzania kushirikiana na Benki ya Dunia ili kuanzisha programu itakayohakikisha kuwa tija inapatikana kwenye sekta nzima ya kilimo na mifugo, lakini pia kuweza kuyafikia masoko kwa mazao yanayozalishwa nchini, hasa yale yenye thamani kubwa duniani.
Dkt. Mpango amefafanua kuwa Benki ya Dunia imeridhishwa na kasi ya mabdiliko inayofanyika katika sekta ya kilimo kwa maana ya uzalishaji kuongezeka, lakini vile vile wakulima wa kati wamezidi kuongezeka.
Aidha, kuongezeka kwa maeneo ya kilimo imewafurahisha wataalamu wa Benki hiyo, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa aina ya mazao yanayolimwa hasa yale yenye thamani kubwa ambayo yanalimwa kwa kasi kubwa sana kuliko ilivyokuwa awali.
Pia Dkt. Mpango alisisitiza kuwa, Benki ya Dunia imeshafanya utafiti wao wa kutosha ambao umeonesha kuna mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo kwa maana ya uzalishaji kuongezeka.
Mhe. Mpango aliishukuru Benki ya Dunia kwa kukubali tena kuleta timu ya wataalamu nchini Tanzania ambayo itakaa na sekta nzima ya kilimo na ufugaji ili kuona ni namna gani hasa Benki ya Dunia itasaidia kuinua sekta hiyo, na kuwasaidia wakulima hasa katika matumizi ya nguvu kazi kwa upande mmoja na kuwaongezea kipato kwa upande mwingine.