- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA IVORY COAST AHUKUMIWA MIAKA 20 JELA
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Cote d'Ivoire(IVORY COAST) na kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na kosa la wizi na utakatishaji wa fedha Nchini humo.
Guillaume Soro ambaye yuko ukimbizini nchini Ufaransa, hakuwepo wakati hukumu hiyo ilipotolewa na mahakama ya Abidjan Jumanne wiki hii.
Guillaume Soro na wanasheria wake wanasema hukumu hiyo ilitolewa na mahakama baada ya kushinikizwa ili kumzuia kuwania nyadhifa ya uongozi nchini humo.
Hivi karibuni Guillaume Soro alitangaza kuwania katika uchaguzi wa urais ujao nchini humo uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Soro anashtumiwa kwamba alitumia fedha za umma takriban Euro Milioni Saba kujinunulia makaazi ya kifahari jijni Abidjan mwaka 2007 alipokuwa waziri mkuu.
Hata hivyo washirika wake wa karibu ikiwa ni pamoja na ndugu zake, wabunge na wafuasi wake wanaendelea kuzuiliwa nchini Cote d'Ivoireb baada ya kukamatwa tangu mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana.
Kulingana na wanasheria wao, kesi hii ni ya kisiasa na ilianza kwa sababu Guillaume Soro, mshirika wa zamani wa Alassane Ouattara, aliachana naye na kutangaza kuwania katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.