Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:41 am

NEWS: WAZIRI MKUU WA UINGEREZA ATOKA HOSPITALI

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson leo ametoka hospitali baada ya kulazwa kwa siku tatu akipatiwa matibabu mara baada ya kuugua ugonjwa wa COVID_19 unaosababishwa na virusi vya Corona. Johnson alilazwa Hospitali ya Mt. Thomas siku 10 baada ya kukutwa na ya virusi vya Corona.

Boris Johnson leaves hospital to continue coronavirus rest at ...

Kimsingi Boris Johnson alifikishwa hospitali siku ya jumapili ya wiki iliyopita ikiwa ni siku 10 baada ya kugundulika ameambukizwa virusi vya Corona wakati huo bado alikuwa na dalili za kukohoa sana na joto kali la mwili. Boris Johnson ana umri wa miaka 55 na kupelekwa kwake kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kumezusha wasiwasi lakini ujumbe wa kumtakia ahueni umemiminika kotoka matabaka mbali mbali ya watu nchini Uingereza na duniani kwa Jumla.

Baada ya kulazwa Bwana Johnson alimtaka waziri wa maswala ya kigeni Dominic Raab kumsaidia pale atakapoweza, msemaji alisema.

Waziri mkuu mwenye umri wa miaka 55 alilazwa katika hospitali ya St. Thomas akiwa na dalili kali za virusi vya ugonjwa huo siku ya Jumapili jioni.

Malkia amekuwa akiarifiwa kuhusu afya ya Johnson kulingana na kasri la Buckingham.

Viongozi mbalimbali duniani akiwemo rais Donald Trump na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamemtumia risala za heri njema bwana Johnson