- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MKUU WA UINGEREZA AGOMA KUJIUZULU
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amepuuza miito ya kujiuzulu, baada ya uamuzi wa mahakama ya juu kwamba hatua yake ya kuahirisha bunge ilikuwa kinyume na sheria. Vikao vya bunge vimeitishwa tena kesho Jumatano.
Uamuzi huo wa mahakama ya juu zaidi nchini Uingereza umeungwa mkono kwa kauli moja na majaji wake wote 11, hali ambayo inazidisha uzito wa uamuzi huo, na matatizo kwa waziri mkuu Boris Johnson. Rais wa mahakama hiyo hiyo, Lady Hale amesema hatua ya serikali ilikuwa na malengo ya kulitatiza bunge kufanya majukumu yake.
''Kwa hiyo mahakama imehitimisha kwamba uamuzi wa kumshauri Malkia kusitisha shughuli za bunge ulikuwa kinyume na sheria, kwa sababu matokeo yake yalilitatiza bunge, au yalilizuia bunge kufanya majukumu yake ya kikatiba, bila sababu yoyote ya msingi.'' Amesema rais huyo wa mahakama ya juu ya Uingereza.
Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya uamuzi huo wa mahakama mjini London, Boris Johnson ambaye yuko mjini New York akihudhuria Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa, amepuuza miito iliyotolewa na wanasiasa mbali mbali wakimtaka ajiuzulu, akisema kuwa kwa maoni yake, uamuzi wa mahakama ya juu haukuwa sahihi.
Amesema, ''Inabidi niseme kwamba napingana vikali na uamuzi wa majaji. Sidhani kama ni sahihi, lakini bila shaka tutasonga mbele, na vikao vya bunge vitafanyika tena.''
Katika hukumu yake, mahakama ya juu imesema hivi sasa ni wajibu wa viongozi wa bunge kuamua muda wa kuanza tena vikao vyao, na tayari spika wa baraza la chini John Bercow, amesema milango ya bunge huko Westminster itafunguliwa kesho Jumatano.