- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania amewatumbua mifuko inayotoa mikopo nakuwataka kurekebisha kiwango cha riba
Dodoma: Serikali imeitaka mifuko ya kijamii ambayo inatoa mikopoko kwa jamii kufanya marekebisho upya ili kuona uwezekano wa kupunguza kiwango cha riba.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa,wakati akizindua Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi,ambapo uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya mashujaa mjini Dodoma.
Majariwa amesema ili kutekeleza sera ya kumkwamua mwananchi katika hali ya umasikini ikiwa ni kupitia katika mifuko ya kijamii ni vyema sasa mifuko hiyo ifanya mapitio upya kwa lengo la kuangalia ni jinsi gani ya kuweza kupunguza riba.
“Ili kuweza kulifanya taifa kufikia sera ya Tanzania ya viwanda ni lazima kufanya linalowezekana kuhakikisha mwananchi wa kipato cha chini anawezeshwa na si kwa kumwekea riba kubwa katika mkopo au kumwekea masharti magumu” alisema Majaliwa.Pamoja na kuwepo mifuko hiyo pia amelitaka baraza la uwekezaji wananchi kiuchumi kufanya tathimini ya kuweza kuiunganisha mifuko hiyo kwa pamoja.
“Nalitaka baraza hili ifikapo Mei 28 mwaka huu nipewe majibu ya nini matokeo ya tathimini ambayo imefanyika kwa ajili ya kuunganisha mifuko ili kuachana na utitiri wa mifuko ambayo ipo kwa sasa” amesema Waziri Mkuu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la uwezeshaji wananchi taifa la Kiuchumi, Dk. John Jingu amesema jitihada sera ya serikali kuwa ya viwanda haziwezi kufanikiwa endapo hapatakuwa na ushirikiano kati ya serikali na wafanya biashara.
“Mifuko hii inatakiwa kujipanga na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na kila mfuko uhakikisha unajenga kiwanda angalau kimoja katika maeneo yao ya kazi” amesema Jingu.