Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 1:01 am

NEWS: WAZIRI MKUU WA ITALIA AMEJIUZULU

Waziri mkuu wa Italia Giuseppe Conte amewasilisha Barua ya kujiuzulu kwa Rais wa nchi hiyo Sergio Mattarella baada ya chama tawala cha LIGI kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani naye(Impeachment) katika muungano huo unaounda serikali ya Italia.

Image result for Giuseppe Conte

Akilihutubia bunge kuhusiana na mzozo huo wa kisiasa uliozushwa na chama cha Ligi, Conte amesema amekabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa rais Sergio Mattarella, ambae ataamua iwapo anataka kuitisha uchaguzi wa mapema ama kujaribu kuunda muungano mpya wa serikali.

Akiwa mkuu wa nchi Matarrella anaweza kumuomba Conte kuendelea na wadhifa huo na kujaribu kutafuta mbadala wa wingi katika bunge, ama kukubali kujiuzulu kwake na kuangalia iwapo baadhi ya viongozi wengine wanaweza kuunda muungano mbadala wa uongozi. Ikishindikana, Mattarella anaweza kulivunja bunge , na kuiweka nchi hiyo katika uchaguzi wa mapema mwezi Oktoba.