Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 12:53 pm

NEWS: WAZIRI MKUU AWATAKA WAFANYABIASHARA KUTOPANDISHA BEI YA BIDHAA KATIKA KIPINDI CHA MWEZI WA RAMADHANI

Dodoma: Serikali imesema imeanza kuandaa utaratibu wa kuuboresha mji wa Dodoma, ikiwemo kuzipitia sheria mbalimbali zilizounda mamlaka ya ustawishaji makao makuu( CDA), kwa lengo la kuzifanyia mapitio na kuziboresha, ili kuweza kuachana na mamlaka hiyo rasmi kwani kwa sasa huwezi kuleta mwekezaji kwa sababu sheria iliyopo imeipa CDA mamlaka pekee ya kumiliki ardhi, hivyo ili kuleta wawekezaji ni lazima kuifuta mamlaka hiyo.

Hayo yamebainishwa bungeni mjini Dodoma na Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh,Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum mkoa wa Dodoma Mh. Kunti Majala aliyetaka kujua ni lini serikali itatekeleza ahadi ya kuifuta mamlaka ya ustawishaji makao makuu(CDA), kama ilivyotolewa na Rais John Pombe Magufuli wakati akiomba ridhaa kwa wananchi wa manispaa ya Dodoma kipindi cha kampeni.

Mh Majaliwa amewataka watanzania kushirikiana na serikali hususani wakati huu tunapoelekea mwezi mtukufu wa ramadhani kuwasihi wafanya biashara wa sukari kutopandisha bei ya Bidhaa hiyo, kwani kwa kufanya hivyo ni kuwaumiza wananchi kwa kuwa serikali inaagiza sukari na kuweka bei ambayo mtanzania yeyote ataweza kuimudu.