Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:21 am

NEWS: WAZIRI MKUU AKASIRISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI BARABARA YA NYAKANAZI

Kigoma: Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameoneshwa kukasirishwa na kasi dhaifu ya ujenzi wa barabara ya Nyanza ya kilomita 50 kutoka Nyakanazi mkoani Kagera hadi Kabingo wilayani Kakonko mkoani Kigoma.

amesema hajaridhishwa kabisa hatua waliyopo kwasababu mradi ulikuwa ni wa kukamilika kwa miaka miwili na sasa mitano.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano Februari 20, 2019 wakati akitokea Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku nne, kuelekea Kagera na kubainisha kuwa mradi huo umekuwa ukisuasua na kuwa nje ya muda.

Amesema mradi huo wa miaka miwili kuanzia mwaka 2014 hadi 2016 lakini mpaka sasa karibu miaka mitano na kazi waliyoifanya ni asilimia 60 huku akiwataka kubadilika na kuchukua hatua za kukamilisha mradi huo.

Mradi huo unaosimamiwa na kampuni ya InterContinental Technocrats (ICT), Waziri Mkuu amesema Serikali imeamua kuwatumia wakandarasi wa ndani ya nchi lakini matokeo ya kazi hayaridhishi na kuwa chini ya kiwango.

"Mnaivunja moyo Serikali iliyoamua kuwaamini na kufanya kazi na makampuni binafsi katika miradi mbalimbali, tukiamua kuchukua wakandarasi wa nje mnapiga kelele na kulalamika, "amesema.

Aidha amewataka kuhakikisha wanaendelea na mradi na kumaliza kwani wakishindwa kufanya hivyo kwa wakati Serikali haitaweza kuwapa kazi nyingine.

"Mradi wa miaka miwili unajengwa kwa miaka mitano, barabara haijawekwa lami, mpaka imeota majani, nimepita hakuna kinachoendelea, Serikali haijaridhishwa na utendaji wenu," amesema Waziri Mkuu.