- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MKUU AAGIZA KUKAMATWA AFISA MANUNUZI
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Singida, - Adili Elinipenda amkamate mara moja Afisa Manunuzi wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, - Francis Muyombo kwa kukiuka taratibu za manunuzi ya Serikali na kughushi nyaraka.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo jana Octoba 6, 2019 wakati akikagua ukarabati wa majengo ya chuo hicho kilichopo wilayani Iramba, ambapo pamoja na mambo mengine amebaini nyaraka zinazoonesha kuwa kitasa kimoja kimenunuliwa kwa Shilingi Elfu Sabini badala ya Shilingi Elfu Ishirini na Tano.
Waziri mkuu Majaliwa alimuhoji afisa huo maswali ya papo kwa papo na Afisa huyo alionesha kuendelea kumdanganya na baada ya muda Wazari mkuu huyo akaamua kutoa kipande chake cha karatasi kilichokuwa na taarifa kamili za manunuzi ya Vifaa hivyo.
“Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 kwa kila chuo ili kufanya ukarabati wa vyuo vya elimu kikiwemo hiki cha kwenu. Ninyi mnanunua vifaa kinyume na utaratibu wa Serikali, hamvikagui, mnaweka tu vitu hafifu ambavyo havidumu. Haiwezekani!”
“Quotation yenu hapa inanionesha mlinunua vitasa 368 vya 3-level kwa gharama ya shilingi 70,000 kila kimoja. Lakini vitasa vilivyoko mlangoni ni vya 1-level ambavyo vinauzwa shilingi 25,000. Haya ni mabweni ya wanafunzi, wanaingi na kutoka kila wakati, ni kwa nini mnaweka vitu cheap wakati mnajua vitaharibika mapema? Maelekezo ya ununuzi wa Serikali yakoje?”
Mara baada ya kumaliza kumuumbua kwa udanganyifu huo Waziri Majaliwa aliagiza hapo hapo kumkamata Afisa Manunuzi huyo.