- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : WAZIRI MAVUNDE AUNGA MKONO MSIMU WA FURSA 2017
Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh.Anthony Mavunde jana alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi rasmi msimu wa fursa 2017 mkoani Arusha.
"Tumehutubia sana,tumesema sana,tumejadili sana,tumepanga mipango sana,sasa ni wakati wa kuachana na dhana hii na kutenda,kufanya, na sio kufanya tu bali kufanya kweli" ..
Ni maneno alionena kwa hisia kali Naibu Waziri Anthony Mavunde akizungumza na mamia ya vijana na vikundi mbalimbali mkoani Arusha Tanzania katika muendelezo wa msimu wa FURSA 2017.
Naibu Waziri Mavunde aliwataka Vijana kuhakikisha wanatumia fursa ya Mifuko 19 ya Uwezeshwaji Wananchi Kiuchumi kama sehemu ya kupatia mitaji ya shughuli mbalimbali za kiuchumi na hivyo kisaidia kuondokana na masharti magumu ya Taasisi za Fedha nyingi.
Aidha aliwashukuru timu nzima ya Fursa chini ya muasisi ndg.Ruge Mutahaba kwa kuzidi kuisaidia yenye kulenga kuisaidia jamii ya kitanzania na serikali kwa ujumla wake kufanikisha maendeleo ya nchi na kuonesha kwa vitendo dhana nzima ya ushirikishwaji.
Mgeni Rasmi ndugu Mavunde aliizungumzia dhana hii ya Fursa na kauli mbiu yake mwaka huu ya Anzia Sokoni akiwataka vijana na watanzania wote wanaotaka kufanikiwa kutokata tamaa na kuwa na malengo yenye tija,kuhakikisha kila siku wanaitumia kuwaza jambo la kufanya na la kuwaletea maendeleo.
Pia,alizungumza ni namna gani serikali mpaka sasa imefanya katika kuhakikisha ina watengenezea vijana mazingira bora na kukazania kwenye mipango iliyopo kwao kuanzia wale walio katika mfumo rasmi wa elimu na wale walionje ya mfumo kuwatengenezea mazingira ya kuendeleza shughuli zao mfano useremala,ushonaji nk kuwapa mafunzo na kuwatengeneza kua bora.
Mwisho aliwashukuru washriki wa Fursa 2017 Umoja wa mataifa kwa kuendelea kushika ajenda hii ya vijana ikiwa kwa mkoa wa Arusha kupitia hilo wanaendelea kutoa mafunzo ya uanagenzi kwa vijana,pia Letshego Tanzania kwa kujidhatiti kuwasaidia vijana kwa mikopo na sapoti nafuu pia ushauri katika safari yao ya kujikwamua kimaisha,wadau wengine ni wazara ya Afya na kampeni yao ya nipo tayari wakihimiza usafi hasa wa maliwatoni kunawa mikono.
Kuelekea kuhitimisha Mh Mavunde alikubaliana na mtazamo wa fursa 2017 wa anzia Sokoni akithibitisha kua katika lolote lile lazima kujua soko linataka nini.