- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MAKAMBA ASEMA RUKSA VIFUNGASHIO VYA KARANGA KUTUMIKA
Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba amesema amekanusha taarifa inayosambaa mitandaoni inayotoka Wasimamizi wa mazingira NEMC kuwa vifungashio vya karanga, Ubuyu etc. marufuku kutumika.
Katika ufafanuzi wake Makamba amesema kuwa hakuna mtu atakayekamatwa kwa kukutwa na vifungashio vya vyakula mfano wa karanga, Ubuyu, kwani kinachokatazwa ni kutumia vifungashio hivyo kubebea bidhaa nyingine.
Kauli hiyo ameitoa Jana kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya kusambaa habari kuwa Serikali imepiga marufuku matumizi ya vifungashio vinavyohifadhia vyakula kama ubuyu, karanga, ice cream na bidhaa nyingine kama hizo ambapo waziri Makamba amesema kuwa taarifa hiyo sio kweli.
“Vifungashio vya bidhaa za vyakula (karanga, ubuyu, etc) havijazuiwa. Kinachozuiwa ni vi-plastic hivi transparent ambavyo huwa vinafungia karanga, ubuyu etc visitumike kuendea sokoni/dukani kubebea bidhaa. Hakuna mtu atakamatwa kwa kuuza karanga kwenye kifungashio cha plastiki” Ameeleza waziri Makamba katika mtandao huo