Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:20 am

NEWS: WAZIRI MAJALIWA KUTUA DODOMA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA VIJANA.

DODOMA: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka ishirini (20)ya siku ya kimataifa ya vijana kwa mwaka 2019 ambayo yatafanyika Jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Meneja programu ya vijana na maendeleo kutoka UNFPA- Tanzania Dk. Majaliwa Marwa, amesema katika maadhimisho yanayowezeshwa na UNFPA, UNESCO, ILO na UNIC yanalengo la kuhakikisha vijana wanajengewa uwezo na kuwa na ubunifu mbalimbali.

Amesema maadhimisho hayo yatashirikisha vijana zaidi ya mia tano(500) kutoka Tanzania bara na visiwani na kwa mwaka huu wamejikita zaidi katika kutilia mkazo kuhusu elimu kwa vijana.

“Mwaka huu ni maadhimisho ya ishirini ya siku ya vijana kimataifa na mwaka huu tumejikita katika elimu ili kuwajengea vijana uwezo na kuwa wabunifu kuweza kujitegemea, dhamira Tanzania iliyopendekezwa kuelekea 2030 TTanzania ya viwanda boresha elimu kwa ajiri ya maendeleo ya vijana” amesema.

Aidha amebainisha baadhi ya shughuli ambazo zitafanyika jijini Dodoma ni pamoja na “Tarehe 15 tutakuwa na kongamano litakuwa na maada mabalimbali ikihusisha ubunifu na afya ya uzazi kwa vijana, na siku ya pili kutakuwa na tamasha litakuwa katika eneo la Chang’ombe eneo lenye mkusanyiko wa vijana wengi na kutakuwa na burudani nyingi” amesema.

Mwenyekiti wa Shirika la RESLESS DEVELOPMENT, chini ya mradi wa Kijana wajibika kwa mkoa wa Dodoma, Ridhiwani Juma, amesema wao kama wenyeji wameweza kuratibu na kuhakikisha vijana wenye mahitaji maalumu nao wanakuwa sehemu ya mmaadhimisho hayo.

Muwakilishi wa vijana ambaye ni katibu Afriyan Tanzania, Seif Ibrahimu amesema kundi la vijana linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kiasi kikubwa.