Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 5:56 am

NEWS: WAZIRI MAHIGA " HATUJAJITOA MAHAKAMA YA AFRIKA"

Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga amesema Serikali ya Tanzania haijajitoa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AFCHPR) kama inavyoeneo bali imeiomba kubadilisha itifaki.

Alisema uamuzi wa kujitoa utakuja baada ya ombi la kubadilisha itifaki hiyo yenye utata katika shughuli za kimahakama kushindikana.

Alisema Serikali imeiandikia barua mahakama hiyo yenye makao makuu yake jijini Arusha kuondoa itifaki hiyo ambayo inapingana na sheria ya Tanzania na kusisitiza kuwa kwa sasa haijajitoa bali inasubiri marekebisho hayo.

“Tunachosubiri kwa sasa ni marekebisho hayo ila ikishindikana basi tutajitoa. Kwa sasa bado hatujajitoa kama inavyosemekana,” alisema.

Miongoni mwa shughuli za mahakama hiyo ni kusikiliza kesi zinazofunguliwa na mashirika yasiyo ya kiserikali au wananchi dhidi ya Serikali.

Mpaka sasa nchi tisa kati ya 30 zilizoridhia itifaki hiyo zimesaini kuwapa uhuru huo wananchi wake kudai haki zao mahakamani pindi Serikali inapowatendea kinyume. Zilizosaini Benin, Burkina Faso, Ivory Coast, Gambia, Ghana, Mali, Malawi, Tanzania na Tunisia.

Zilizoridhia ni Algeria, Burundi, Cameroon, Chad, Comoros, Kongo, Gabon, Kenya, Libya, Lesotho, Msumbiji, Mauritania, Mauritius, Nigeria, Niger, Rwanda, Jamuhuri ya Kidemokrasia Sahrawi, Afrika Kusini, Senegal, Togo na Uganda.

Miongoni mwa kesi za Tanzania ambazo zimewahi kuamriwa kwenye mahakama hiyo ni ya mwanamuzi maarufu Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Johnson Nguza au Papii Kocha.

Babu Seya na wanaye walihukumiwa kufungwa maisha na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2004. Walikata rufaa Mahakama Kuu wakashindwa, Mahakama ya Rufani ikawaachia huru watoto wawili lakini Babu Seya mwenyewe na Papii Kocha wakaendelea kutumikia adhabu hiyo.

Mwaka 2015 walikimbilia katika mahakama hiyo na Machi 23, 2018 ikakubali kukiukwa kwa baadhi ya haki zao hivyo kuamuru waachiwe ingawa walishapata msamaha wa Ra